Mwongozo mfupi wa skrini wa matiti

Karatasi hii inatoa muhtasari mfupi wa Skrini ya Matiti (BreastScreen) Queensland. Inafafanua ni nani anayeweza kuwa na skrini ya matiti katika programu, skrini ya matiti inahusisha nini, na jinsi ya kuomba miadi.

Mwongozo mfupi wa skrini wa matiti [PDF 253.49 KB]

Ni kitu gani kinachotokea kwenye miadi ya uchunguzi wa matiti

Video hii inaelezea mchakato wa kufanya skrini ya matiti nasi. Inashughulikia:

  • jinsi ya kujiandaa kwa miadi yako
  • jinsi matiti yako yatachunguzwa
  • nini kitatokea baada ya miadi yako.

Skrini ya matiti inaweza kusaidia kupata saratani katika hatua za mwanzo,
kukupa chaguzi zaidi za matibabu.

Hapa katika BreastScreen Queensland, tunatoa skrini ya matiti bila malipo kuzunguka jimbo kwa wanawake wenye miaka 40 na zaidi ambao hawajaona mabadiliko yoyote katika matiti yao. Skrini ya matiti ndiyo yenye ufanisi zaidi kwa wanawake kati ya miaka 50 hadi 74, na tutakutumia mwaliko kila baada ya miaka 2 unapokuwa katika kundi hili la umri.

Unapotembelea kwa miadi yako, tafadhali usivae unga wa talcum au deodorant kwani inaweza kuathiri skrini yako ya matiti. Tunashauri unavaa juu na chini tofauti ili nusu yako ya chini ifunikwe wakati wa skrini.

Inasaidia kama ukifika dakika 10 mapema. Wakati ukifika, utakaribishwa na na mtu wetu wa mapokezi mkarimu. Watakuomba ujaze baadhi ya fomu na angalia kadi yako ya Medicare.

Mpiga picha (Radiographer) wetu wa kike itakupeleka kwenye chumba cha uchunguzi na kueleza kitakachotokea. unaweza, kumuuliza maswali yoyote unaweza kuwa nayo. Atatumia mashine maalum ya X-ray kutafuta saratani ndogo sana ambayo haiwezi kuonekana au kuhisiwa na daktari wako.

Unaweza kuwa na wasiwasi kuwa skrini itachukua muda au uchungu, lakini kwa kawaida ni haraka na kutokuwa na raha kidogo tu. Unaweza kuuliza mpiga picha wako (radiographer) kusimamisha wakati wowote.

Bado atakuoomba uondoe nguo yako ya juu na brauzi na ataelekeza matiti kwenye mashine na weka shinikizo kwa sekunde chache ili kupata picha.
Hii basi itarudiwa kwa matiti mengine. Atachukua X-rays nne, mbili za kila matiti.

Picha za skrini ya matiti yako itasomwa kwa kujitegemea na walau madaktari wawili wenye utalaamu wa hali ya juu. Wanawake wengi hupata majibu yako ndani ya wili nne. Ukitupa maelezo ya daktari wako, tutawatumia nakala pia.

wanawake 95 kati ya 100 hupata matokeo ya kawaida ya skrini ya matiti
bila saratani ya matiti kupatikana. Wanawake watano kati ya 100 wanahitaji vipimo zaidi. Lakini ukianguka katika kundi hili, haimaanishi kuwa una saratani. Hii ina maana tu kwamba kitu kinahitaji kutazamwa kwa karibu katika Kliniki yetu ya Tathmini.

Unaweza kutembelea itachukua chini ya dakika 30, na wakati huo, wafanyakazi wetu wenye uzoefu na kukaribisha itachukua huduma bora yako wewe.

Hivyo, kama uko zaidi ya miaka 40,chukua hii huduma yetu ya kupata skrini ya bure ya matiti. Na kama una miaka 50 mpaka 74, tutakualika uendelee kutujulisha kuhusiana na skrini ya matiti kwa sababu ugunduzi wa mapema unatoa njia nyini za matibabu na hiyo inaleta tofauti kubwa.

Agiza skrini ya matiti leo.

Tuna zaidi ya vituo 260 kuzunguka Queensland, baadhi ya hivyi masaa yasiyo ya kazi.

Kwa habari zaidi au kufanya miadi, tembelea breastscreen.qld.gov.au au pigia kituo cha mahalo pako cha BreastScreen Queensland Service kwa 13 20 50.

Last updated: June 2024